Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amepongeza maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi huo ambapo ameeleza kwamba unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mapema kabla ya Julai 25 mwaka huu ili uweze kutumika kwa ajili ya shughuli za Mashujaa.

Amesema, mpaka sasa hatua iliyofikiwa ni ujazaji wa udongo na kushindiliwa huku akimsisitiza mkandarasi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kuzingatia ubora na uimara wa miundombinu ndani ya muda uliopangwa.

“Kazi inaendelea vizuri kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Mashujaa maeneo mbalimbali yameshajazwa udongo na kushindiliwa hivyo tunaamini mkandarasi wetu SUMA JKT atafanya kazi nzuri,” Amesema Dkt. Yonazi.

Aidha kuhusu mfumo wa maji taka amebainisha kuwa itajengwa katika hali ya bora ili kuhakikisha Mji wa Serikali unakuwa katika mandhari nzuri na ya kuvutia kulingana na malengo ya Serikali ya kukamilisha Mji wa Serikali.

Museveni apata maambukizi Uviko-19, asema yupo fiti
Azam FC yasitisha usajili Singida Big Stars