Ushahidi wa vina saba (DNA) uliotokana na upimaji wa jasho la shati inayohusishwa na tukio, imefanikiwa kumshika Russel Bishop, mtuhumiwa wa ubakaji wa watoto wawili wenye umri wa miaka 9, lililofanyika miaka 32 iliyopita nchini Uingereza.

Bishop mwenye umri wa miaka 52, anakabiliwa na kesi ya ubakaji na mauaji ya watoto Nicola Fellows na Karen Hadaway, anayodaiwa kutekeleza Oktoba 9, 1986. Watoto hao walikutwa wakiwa wamekufa siku moja baada ya kupotea nyumbani kwao.

Bishop alikamatwa kama mtuhumiwa wa kwanza lakini ilimbidi kusubiri hadi teknolojia mpya ya DNA ianze kutumika ili kubaini ushahidi wa jasho la shati kwa kulinganisha na jasho la shati iliyokutwa kwenye eneo la tukio la mauaji iliyowagusa watoto hao.

Jopo la majaji, wiki hii limeambiwa kuwa vipimo vya DNA vimeonesha mfanano wa jasho la shati ambayo Bishop aliivua alipokuwa anaelekea nyumbani kwake baada ya tukio hilo.

“Tunaweza kusema Mahakama ihitimishe kuwa shati lililochukuliwa vipimo ni la mtuhumiwa, na kwamba limebainika kuwa lilizigusa nguo za watoto kwa mara ya mwisho ambayo ni wakati wa tukio hilo la mauaji,” mwendesha mashtaka aliliambia jopo la majaji.

Mwendesha mashtaka huyo alikumbushia tukio la utekaji, ubakaj na jaribio la kumuua mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba la mwaka 1990, ambalo Mahakama ilimkuta Bishop na hatia  na anatumikia kifungo hadi mwaka 2007.

Bishop amekana tuhuma hizo dhidi yake, na kesi hiyo maarufu inaendelea.

Polisi waeleza watekaji walivyoishi na Mo Dewji, ‘walimfunga’
Familia ya Mo Dewji yaeleza alivyopatikana, afya yake

Comments

comments