Uongozi wa Dodoma Jiji FC, umeweka wazi kwamba, timu yao ipo katika maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Juni 06, mwaka huu kwenye Dimba la Majaliwa mkoani Lindi.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, amesema: Kwa asilimia mia moja maandalizi yanaenda vizuri, wachezaji wana ari na morali kwa ajili ya kupambana, wanauchukulia mchezo huu kwa umuhimu mkubwa ambao tunatakiwa kuondoka na alama tatu ili kuwa kwenye nafasi nzuri.

“Mchezo utakuwa mgumu, tukiangalia wapinzani wetu wako nafasi ya juu, sisi tutaingia kwa tahadhari kubwa kuwaheshimu ili tuweze kupata alama tatu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo huu maana malengo yetu ni kuhakikisha tunapambana kupata matokeo mazuri kwenye mechi zilizobaki kutokana na kila timu inapambana kujiweka kwenye mazingira Bora na sisi tutatumia changamoto hiyo ili tuzidi kujimarisha.”

Expressway Kibaha - Chalinze - Moro ipo mbioni - Serikali
Morogoro waibuka na Tuzo za Filamu