Asia Said Ali (50) Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA, Kata ya Palanga Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kupigwa mshale na Haruna Ali Kimata (35).

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema tukio hilo halihusiani na siasa, Mume wa marehemu alikuwa na migogoro na muuaji ambapo tayari ametiwa mbaroni.

Imeelezwa kuwa Haruna alitaka kumpiga mshale Iddi Masale (55) ambaye ni Mume wa marehemu ila ulimkosa na kumpiga Asia Mgongoni na kufariki muda mchache baada ya kufikishwa hospitalini.

Imeelezwa kuwa marumbano hayo yalitokea baada ya Iddi Masale kuingiza Mifugo kwenye Shamba la Alizeti la Haruna ndipo alikwenda kumvizia usiku ili kutimiza azma yake hiyo.

Kaimu afisa habari wa CHADEMA kanda ya kati, Juma Omary amesema mzishi ya mwenyekiti huyo yatafanyika leo Julai 23, 2020.

Watumishi tisa TAKUKURU wasimamishwa kazi
Hatma ya Alliance FC, Ndanda FC kujulikana leo