Dogo Janja ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Kidebe’ amefunguka na kutangaza rasmi kuwa ana mpango wa  kuoa na kusema kwamba muda si mrefu anaweza kuvuta jiko na kuweka ndani.

‘Yah ni  kweli nataka kuoa muda si mrefu nitavuta jiko hivyo siwezi kusema ni lini, ila suala hilo lipo kwenye mchakato” alisema Dogo Janja.

Kwa upande wa Madee ambaye ni mlezi wa Dogo Janja kimuziki na katika maisha ya kila siku alisema kuwa kitendo cha Dogo Janja kutaka kuoa kabla yake itakuwa kama dharau hivyo anapaswa kusikilizia kwanza mpaka yeye atapooa.

“Ha ha ha ha Dogo Janja kuoa kabla yangu itakuwa kama dharau aiseee anapaswa kusubiri kwanza mimi nifanikishe jambo hilo ndiyo yeye afuate” alisema Madee.

Dogo Janja alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja kutokea Manzese.

Raymond: Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview
Ndanda FC Yapoteza Ajira Ya Rogasian Kaijage