Tafiti zimebainisha kuwa katika mataifa yaliyoendelea, Marekani ni moja ya nchi ambayo ina kiwango kidogo sana cha kinamama kunyonyesha watoto wao pindi tu wanapozaliwa, katika kutatua tatizo hilo baadhi ya miji imeamua kuwalipa wakinamama wanonyesha watoto wao angalau mpaka wiki sita.

Ambapo malipo hayo hufanyika kwa vocha wazazi hupewa vocha kuanzia Dola 80 sawa na shilingi 180,000 za Kitanzania mpaka Dola 200 sawa na Shilingi 450,000 ya Kitanzania za kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali.

Kufuatia hatua hiyo kumefanya mabadiliko makubwa katika swala zima la unyonyeshaji ambapo utolewaji wa ofa hiyo imepelekea kina mama wengi wawe na mwitiko wa kunyonyesha watoto wao na kudai malipo hayo.

Hata hivyo utolewaji wa vocha hizo umetumika kama namna ya kutoa shukurani kwa kina mama kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwanyonyesha watoto wao wakiwa bado wadogo ili kuleta vizazi vyenye akili ya kuijenga nchi kwani tafiti zimebainisha kuwa watoto wengi wanaokosa maziwa kutoka kwa mama zao hukosa uwezo mzuri wa kufikiri na ubongo kudumaa.

Aidha tatizo la kina mama kutowapa watoto wao maziwa limekuwa tatizo kubwa katika nchi za watu walioendelea na famailia zilizo na uwezo wa kutumia maziwa ya kopo, ila si jambo zuri kwa watoto kwani kuwakosesha mazima ya mama ni kuwakosesha haki yao ya msingi kama watoto.

Mtoto anapaswa kunyonya maziwa ya mama kuanzia mwaka’ 0 mpaka miezi 6 mfululizo bila kuchanganya na chakula kingine chochote.

 

Video: Makonda awapa onyo kali wasichana wa mkoa wake
Guardiola amwaga wino tena Man City