Daktari wa mgombea urais nchini Marekani Dr Harold Bornstein amesema alitumia dakika tano kuandika barua ya kuidhinisha afya ya mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald Trump.

Barua ya Dr Bornstein ilisema Bw Trump, mwenye umri wa miaka 70, atakuwa “ndiye mtu binafsi mwenye afya aliyewahi kuchaguliwa kuwa rais”

Wiki mbili kabla ya kuandikwa kwa waraka huo, Bw Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kwamba “nilimuagiza daktari wangu wa muda mrefu kutoa, ripoti kamili ya afya yangu katika kipindi cha wiki mbili”, akiongeza kuwa itaonesha “usahihi na baadae Bw Trump alionyesha waraka ulioidhinishwa na Dr Bornstein, ambaye alikabiliwa na maswali kuhusu lugha ya mvuto aliyoitumia kwenye waraka huo.

Aidha daktari huyo wa hospitali ya New york ya Lenox Hill, anasema huenda alitumia maneno ya kuvutia zaidi ili kuwafurahisha watu wa kampeni ya Donald trump”

Hata hivyo bw Trump atakuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani, kama atashinda uchaguzi wa mwezi Novemba.

Afya za wagombea hao wawili zimekuwa ni suala linaloangaliwa katika kampeni, huku Bw Trump akirejea na madai yake kwamba hasimu wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton hana afya nzuri.

Bi Clinton alijibu kile alichosema kuwa ni madai yasiyo na msingi, na Bw Trump amekabiliwa na ukosoaji kuhusu namna anavyomshambulia Bi Clinton kuhusu suala hilo

Jenister Mhagama Azindua Taasisi Ya Ujasiliamali Na Ushindani Tanzania(TEEC)
Serikali Kuboresha Ufundishaji Shule Za Awali,Msingi Na Sekondari