Kiungo wa Manchester United, Donny van de Beek, 24, ameripotiwa kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka kwenye timu hiyo katika dirisha lijalo la majira ya baridi na katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa amebadilisha wakala.

Fundi huyo kutoka Uholanzi anawindwa na Everton, Newcastle na Juventus ambazo zilitaka kumsajili katika dirisha lililopita, lakini hazikufanikiwa.

Kushindwa kuondoka kwenye viunga hivyo katika dirisha lililopita ndiko kumemfanya Van de Beek ajiunge na kampuni nyingine ya uwakala ambayo anaamini itakamilisha dili lake la kusepa Manchester United.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2023 na amekuwa hapati nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United hali inayosababisha atamani sana kuondoka kwa kuhofia kwamba atapoteza namba kwenye timu ya taifa.

Gomes aikana Young Africans
Rayvann achukizwa na chuki za wasanii Tanzania.