Naibu waziri wa afya na Mbunge wa Nzega, Dr. Kigwangalla, amewasha moto katika mtandao wa kijamii wa twitter kwa kutoa meneno makali yaliyowachachua baadhi ya wafuasi wake na kuamua kumjibu.

Jana kupitia mtandao wake wa twitter Dr. Kingwangala ambaye ni naibu waziri wa afya, ameandika hivi,

”Watu wetu wanaangamia kwa kukosa maarifa! Baadala ya kuyatafuta, hupinga kila kitu kwa hoja za kufuata mkumbo! Wakiitwa Nyumbu hulalamika”.

Mmoja kati ya waandishi wakongwe wa vitabu vya adithi, Richard Mabala aliyepata umaarufu wake nchini kupitia kitabu cha hadithi ya Hawa The Bus Driver na Mabala the farmer kinachotumika katika elimu ya sekondari kwa madarasa ya chini, Richard Mabala alimjibu Dr. Kingwangalla na kusema.

”kuwafananisha watu na wanyama kila wakati kunaweza kusababishwa na matumizi ya dawa za kulevya pia”. ameandika Richard Mabala wakati akijibu twiti ya Dr. Kingwangalla.

Nini maoni yako kuhusu alichozunguzma Dr. Kingwangalla, na Je alichosema Mwandishi na mwalimu Richard Mabala kinaukweli wowote?.

Manji na wenzake wazidi kusota jela
Mahakama yatengua kauli zuio la kuapisha wabunge wapya CUF