Drake amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu namna alivyowahi kutaka kufunga pingu za maisha ya Rihanna, walipokuwa wapenzi miaka kadhaa iliyopita.

Mkali huyo wa ‘In My Feelings’ amefunguka kwenye mahojiano aliyofanya na LeBrone James pamoja na Maverick Carter kwenye kipindi cha ‘The Shop’ cha HBO wikendi hii.

Ni kama penzi la Rihanna lilimkuna kunako rapa huyu ambaye amesema kuwa anatamani kungekuwa na simulizi la hadithi ya uhusiano unaoishia kwenye ndoa na kutengeneza familia na Rihanna.

“Kama ujuavyo maisha hutengeneza umbile na kukufundisha masomo, niliishia kwenye hali hii ambayo sina simulizi la hadithi za zamani; kama ‘Oh, Drake alianzisha familia na Rihanna na imekuwa kamilifu,” alifunguka.

“Zinaonekana kuwa hadithi nzuri kwenye magazeti,” Drake alikumbuka walivyokuwa wakiandikwa. “Hata hivyo, kuna wakati na mimi nilikuwa natamani hiyo itokee [na Rihanna],” aliongeza.

Drake na Rihanna walikuwa kwenye uhusiano wa mapenzi tangu mwaka 2009, lakini uhusiano wao ulikuwa kama tetesi hadi Drake alipoweka wazi mwaka 2016 alipokuwa anamkabidhi mrembo huyo tuzo ya Video Bora kwenye Tuzo za Video za Muziki za MTV (MTV VMAs).

“Huyu ni mwanamke ambaye nimekuwa kwenye uhusiano naye tangu nikiwa na umri wa miaka 22,” alisema Drake. Wawili hao waliachana rasmi baadaye mwaka huohuo.

Uhusiano wa Drake na Rihanna uliambatana na kufyatuliwa kwa ngoma kali kama ‘Work’, ‘Too Good’,’What’s my Name’ na ‘Take Care’.

Katika hatua nyingine, Drake alieleza kuhusu uhusiano wake na mama wa mtoto wake, uhusiano ambao alidai umemfanya kuwa baba wa mtoto lakini anajivunia na hatamlaumu mama mtoto wake kwa lolote lililotokea

Amesema hataki dunia au mtoto wake huyo wa kiume kutompenda mwanamke huyo ambaye anaendelea kuwasiliana naye kwa mengi kuhusu malezi ya mtoto wao.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 16, 2018
Kanye amzawadi kiatu Museveni

Comments

comments