Umewahi kumiliki kitu ulichokuwa unakiazima kwa watu wakati hauna pesa??

Hii imetokea kwa rapa Dizzy Drake ambaye hatimaye amefanikiwa kumiliki gari alilokuwa akilikodi kutoka kwa jamaa zake takribani miaka kumi na nne (14) iliyopita, wakati akipambana kutafuta nafasi ya kufanikiwa kimuziki.

Drake sasa analimiki gari hilo baada ya meneja wake na Dj future the Prince, kuamua kumnunulia gari hilo aina ya Rolls Royce Phantom toleo la mwaka 2007 na kumpatia kama zawadi kwenye sherehe ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumza kuhusu mapokezi yake juu ya zawadi hiyo, Drake amesema alikuwa akilikodi gari hilo kwa kiasi cha pesa Usd 5,000 ambazo ni sawa na 11.5 Milioni kwa mwezi ikiwa ni sehemu ya kuilinda brand yake na kutegeneza thamani yake mtaani katika kipindi alichokuwa akitafuta nafasi yakufikia malengo yake.

Rapa Drake kwa sasa ni mmoja wa wasanii wenye utajiri mkubwa akiwa anashikilia nafasi za juu kwenye chati mbali mbali za muziki Duniani.

Biashara United yakana tuhuma za rushwa
Simba SC yapelekwa Zambia