Drake amekosa furaha ya kuendelea kuwa na uhusiano wa kibiashara na Jordan ambayo ameshirikiana nayo tangu mwaka 2013 akitangaza mavazi yake, na sasa amehamishia ndoto zake kwenye kampuni ya Adidas.

Rapa huyo ameipigisha hatua Jordan kwa kipindi cha miaka minne akiimba mara kadhaa kwenye nyimbo zake na kuwafanya mashabiki wake kuifanya chaguo la kwanza kwenye manunuzi yao ya mavazi hasa viatu.

Alifanikisha kutangaza kwa kishindo matoleo mapya ya Jordan ambayo yamepigiwa debe mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Nice Kicks, Drake ameshaanza mazungumzo na adidas na anaweza kusaini mkataba muda wowote.

Kama rapa huyoambaye jina lake la kuzaliwa ni Aubrey Graham atasaini na Adidas, ataungana na Kanye West, Pusha T na Pharrell Williams kwenye biashara hiyo.

T.I afunguka mpango wa kudhibiti umiliki silaha, 'watatuonea'
Zitto aachiwa huru kwa dhamana ya mamilioni