Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC imeishutumu Rwanda kwa shambulio baada ya nchi hiyo kuthibitisha kuwa vikosi vyake viliifyatulia risasi ndege ya kivita, kutoka DRC ambayo ilikiuka sheria ya anga lake.

Kwa mujibu wa Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ilionyesha risasi ikielekea kwenye ndege ya kijeshi ya angani, kabla ya kulipuka wakati ikiendelea kuruka.

Tukio hilo, ni mzozo wa hivi punde kati ya nchi hizo mbili ambazo uhusiano wao umezorota kutokana na uasi wa waasi na DRC imekanusha kuwa ndege hiyo ilikuwa sheria za anga za Rwanda, ikisema kuwa ilikuwa ikiruka ndani ya ardhi ya Kongo.

Ndege hiyo ikitua katika mji mkuu wa Goma-DRC bila kupata madhara makubwa. Picha ya Pars Today.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa Ndege hiyo ilitua katika mji mkuu wa jimbo la Kongo Goma bila kupata madhara makubwa huku DRC, wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi yakiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 ambalo liliteka miji na vijiji kadhaa mashariki mwa DRC mwaka jana.

Wakati huo huo Papa Francis anatayarisha ziara ya DRC, nchi yenye imani ya Kikatoliki, kuanzia Januari 312, 2023 ikitafsiriwa kuwa ziara hiyo itatuliza hali ya wasiwasi mashariki mwa nchi hiyo.

Zaidi ya waumini milioni moja, wanatarajiwa kuhudhuria misa ya wazi katika uwanja wa ndege wa Ndolo mjini Kinshasa tarehe Februari 1, 2023 wakati Papa atakapokutana na wahanga wa mzozo huo.

Wazazi washauriwa kuwagua watoto sehemu za siri
CCM Iringa yataka Watoto wa kiume kuwekewa ulinzi