Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuondokana na ugonjwa wa Ebola baada ya siku zaidi ya 40 bila kuripotiwa kwa ugonjwa huo.

Mlipuko wa hivi karibuni kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ulikuwa wa tatu katika kipindi cha miaka miwili.

Mwanzoni mwa mwezi Juni, wagonjwa kadhaa walipatikana na ugonjwa huo katika eneo la Mbandaka ambapo watu 130 waliambukizwa ugonjwa huo, huku 55 kati yao walifariki dunia.

Visa vya ugonjwa huo eneo la Mbandaka vilibainika wakati mlipuko wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo unakaribia kufikia ukomo wake.

Shirika la Afya Duniani limeidhinisha chanjo iliyotolewa na kampuni ya dawa ya Merk ambayo imetolewa kwa watu 400,000 kote nchini humo.

Mwezi uliopita, Shirika la Dawa nchini Marekani limeidhinisha dawa ya Inmazeb kama tiba ya Ebola, baada ya kufanyiwa majaribio huko Congo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikikabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa Ebola kwa kufuatana tangu mwaka 2018 na zaidi ya watu 2,000 wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Kaseja na wenzake warejea KMC FC
Uganda: Bobi Wine akamatwa na Polisi