Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) leo jumatatu Agosti 31 imetangaza kiasi cha pesa ambacho kitatakiwa kulipwa ,kupata kibali cha kurusha Drone katika anga la Tanzania .

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCAA Hamza Johari amesema kuwa hakutakuwa na kibari cha kurusha Drone nchi nzima

“Usajili wa Drone ni Dola 100 ambayo utalipa kila mwaka, hakuna kibali cha kurusha Drone nchi nzima ni kila Mkoa, hivyo kama umesajiliwa Dar es Salaam ukihitaji kwenda Mkoa mwingine kikazi utakuja kuomba kibali tena,” amesema Hamza Johari

katika hatua nyingine Jeshi la Polisi nchini kupitia msemaji wake David Misime limesema kuwa urushwaji wa Drones kwenye Maeneo ya Nchiunaweza kuihujumu nchi .

“Drone zinaweza kutumika kuihujumu nchi kwa kuchukua taarifa kwa nia ovu, hivyo ukikamatwa unaiendesha bila kibali ni kosa la jinai kama yalivyo makosa mengine,” amesema Misime.

Bomu laua mwanafunzi wa darasa la pili
Uchaguzi Mkuu 2020: Polisi kushirikiana na jamii