Kikosi cha Azam FC leo Jumamosi (Septemba 11) kitamkosa Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Prince Dube, kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Horseed FC kutoka Somalia.

Azam FC watakuwa na kazi nzito ya kusaka namna ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo, wakianzia nyumbani Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, mishale ya saa moja jioni.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari na mawasilino ya Azam FC imeeleza kuwa Mshambuliaji wao hatari, Prince Dube hatakuwa sehemu ya kikosi cha wawakilishi hao wa Tanzania, kutokana na kuwa majeruhi.

Taarifa hizo zimeongeza kuwa, kwa sasa Dube yupo nchini Afrika Kusini ambapo amefanyiwa upasuaji, na anaendelea vizuri.

Dube ambaye msimu uliopita alitupia mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma sita.

Miaka 20 ya mashambulizi ya Septemba 11 Marekani
Simba SC yavunja ukimya, ujio wa Hitimana Thiery