Beki wa Kulia wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC David Kameta ‘Duchu’, huenda akajiunga na klabu ya Mbaye Kwanza FC kwa Mkopo.

Mbeya Kwanza FC itakayoshiriki Ligi Kuu msimu ujao 2021/22 kwa mara kwanza, itanufaika na usajili wa beki huyo kwa makubaliano ya Mkopo.

Taarifa zinaeleza kuwa Duchu ataondoka Simba SC kufuatia changamoto ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC, kutokana na umahiri wa Shomari Kapombe aliyecheza asilimia kubwa ya michezo ya klabu hiyo msimu wa 2020/21.

Pia inaelezwa kuwa usajili wa beki wa kulia wa KMC FC Israel Patrick Mwenda ndani ya Simba SC, nao unatoa msukumo kwa Duchu kutafutiwa nafasi ya kuitumikia Mbeya City kwa Mkopo.

Hata hivyo endapo Duchu atasajiliwa Mbeya Kwanza FC atakuwa na uhakika wa kucheza mara kwa mara tofauti na sasa akiwa Simba SC.

Duchu alisajiliwa Simba SC akitokea Lipuli FC mwanzoni mwa msimu wa 2020/21.

Lazima mahabusu wapimwe -Prof. Makubi
Vandenbroeck aikataa Simba SC usajili 2021/22