Siku moja baada ya kumuomba msamaha Shetta kwa kumwagia matusi ya nguoni akimtuhumu kutumia jina lake ‘Mamba’, Rapa Dudu Baya aka Mamba ametoa maoni yake tata kuhusu hali ya rapa mwenzake Chidi Benz anayekabiliwa na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea kupitia Ladha 3600 ya E-FM, Dudu Baya amesema kuwa Chid Benz hapaswi kusaidiwa balia anapaswa kuachwa hadi apoteze maisha ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, maoni ya Dudu Baya yalipingwa vikali na rafiki yake wa karibu, Mwana FA ambaye aliyaita mawazo ya kijinga na kiupuuzi.

“Watu wanafanya makosa ila hatuwezi fikia kutamka maneno kama hayo kiubinadam,” alisema Mwana FA.

Ramires Afichua Siri Ya Kuondoka Chelsea
Dk. Shein amtosa Rasmi Maalim Seif