Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Dwight Yorke amesema wachezaji sita tu wa sasa wa timu hiyo ndiyo wako salama mbele ya kocha mpya, Jose Mourinho kubaki Old Trafford.

Mreno huyo amerithi mikoba ya Mholanzi, Louis van Gaal baada ya msimu huu na anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha timu hiyo hususan baada ya kuripotiwa kupewa fungu la Pauni Milioni 200 za kusajili wachezaji wapya.

Yorke, aliyekuwamo kwenye kikosi cha Man United kilichotwaa mataji matatu mwaka 1999, mawili ya England na moja la Ligi ya mabingwa, amewataja wachezaji hao kuwa ni David de Gea, Anthony Martial, Michael Rashford na Nahodha Wayne Rooney ndiyo wanaweza kubaki mbele ya kocha wa zamani wa Chelsea msimu ujao.

Akizungumza katika mahojiano maalum na 888sport, Yorke amesema: “Kila mmoja mmoja anaruka ruka, lakini ni tetesi tu kwenye vyombo vya habari. Tunafahamu fika juu ya (Juan) Mata na Jose na hilo halina mabadiliko,”

“Kuna wachezaji wachache ambao ni wa Manchester United lakini wapo huko,”ameongeza mkali huyo wa mabao wa zamani wa Mashetani Wekundu, enzi zake akicheza pamoja na Andy Cole.

“Wamecheza chini ya kiwango na hakuna aliye salama ukiondoa De Gea, Martial, Rashford na Rooney. Kila mmoja baina yao wataangalia juu ya mabega yao,”

Katika hao wachezaji wanne, Yorke binafsi amevutiwa zaidi na mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa, Martial ambaye amemaliza msimu akiwa mfungaji bora wa klabu.

Wabunge wa Upinzani wamsusia tena Naibu Spika
Manji Na Makamu Wake, Clement Sanga Kuchukua Fomu Leo