Idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko wa Ebola nchini Uganda imeongezeka na kufikia watu 11 ambapo wengine 24 wakiwa wamelazwa katika kituo cha afya na maafisa wa serikali wakijaribu kuzuia ugonjwa huo usienee maeneo mengine.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Emmanuel Ainebyoona amesema visa vyote vipya na vifo vimetokea katikati mwa nchi ya Uganda katika Wilaya ya Mubende ambapo mpaka sasa kesi zilizothibitishwa zimefikia 11 na mawasiliano 58 ya wahasiriwa yameorodheshwa ili kuwafuatiliwa kwa ukaribu.

Hata hivyo, Maafisa wa serikali wa timu ya kukabiliana na Ebola wameonya kuwa visa vya maambukizi huenda vikaendelea kuongezeka, kwa sababu ya kuchelewa kwa mwitikio na ujuzi mdogo kuhusu kiwango cha kuenea kwa ugonjwa huo.

Serikali inasema dalili za Ebola ni sawa na za malaria na typhoid na maambukizi yanaweza kudhaniwa kuwa ni ugonjwa wa kawaida.

Takwimu za hivi punde, kutoka kwa Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kuna visa 11 vilivyothibitishwa vya kuambukizwa kwa Ebola na vifo vitatu vilivyothibitishwa na kwamba takriban vifo sita kati ya vinavyowezekana vilitokea katika jamii.

Septemba 22, 2022, Kamanda wa tukio la Ebola, Dkt. Henry Kyobe alisema katika mahojiano kwamba ugonjwa huo ulianza kuenea mwanzoni mwa mwezi huu, lakini mlipuko huo ulithibitishwa rasmi siku Jumanne Septemba 20, 2022 ikimaanisha kuwa ugonjwa huo umekuwa ukienea kwa wiki.

Alisema, “Kuna muda kidogo kutoka kwa kesi za awali na wakati tulithibitisha na kutangaza kuzuka kwa ugonjwa huu, dalili za Ebola ni sawa na za malaria na typhoid na maambukizi yanaweza kudhaniwa kuwa ni ugonjwa wa kawaida hivyo watu waonapo dalili hizo ni vyema wakawahi vituo vya afya kuchunguza afya.”

Serikali yakubali mchango wa Madhehebu sekta ya Afya na Elimu
Makamu wa Rais athibitisha baba yake kutetea kiti cha Urais