Mwanamuziki nyota kutoka nchini Uganda, Eddy Kenzo ameingia kwenye orodha ya nyota wengine wakubwa kutoka mataifa mbali mbali waliotajwa kuwania tuzo za Grammy za mwaka 2023 akitajwa kuwania kipengele cha ‘Best Global Music Perfomance kupitia wimbo wake uitwao ‘Gimme love’ aliomshirikisha Mattbworld.

Eddy Kenzo, ambaye anauwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki ataungana na wasanii wengine kutoka Afrika akiwemo Tems, Angelique Kidjo, Burna boy, Nomcebo, pamoja na RO ckydawuni wanaowania pia Kipengele cha Best Global Music Performance, Song Of The Year.

Kwa upande wa nyota Burna Boy, yeye nu mmoja wa wasanii waliotajwa kwenye zaidi vipengele viwili ambavyo ni”Best Global Music Performance” kupitia wimbo wake ‘Last Last’ pamoja kipengele kingine ambacho ni ‘Best Global Music Album’ Love Damini.

Mwanamuziki, Eddy Kenzo. Picha ya Instagram.

Msanii mwingine ni mrembo Tems ambaye naye ametajwa kwenye vipengele Viwili ambavyo ni’Best Melodic Rap Performance’ Kupitia wimbo alioshirikishwa na Future pamoja na Drake ‘Wait For You’ pamoja na “Best Rap Song ‘Wait For You’.

Grammy 2023, zitakuwa ni tuzpo za 65 na tano tangu kuanza kutolewa kwake, amabapo awamu hii hafla ya utolewaji wa tuzo hizo itafanyika Februari 2023 katika ukumbi wa Crypto mjini Los Angeles nchini Marekani.

Wasanii wanaowania tuzo za Grammy 2023
Mangungu achimbwa mkwara Simba SC