Mwanamuziki Edrisah Musuuza maarufu kwa jina la kisanii Eddy Kenzo, ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrima kwenye kupengele cha mwanamuziki bora wa kiume ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwenye kinyang’anyiro hicho Eddy Kenzo alikuwa akichuana vikali na wasanii kadhaa wenye kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Afrika mashariki akiwamo msanii Diamond Platnumz, Harmonize, Darassa, Meddy (Rwanda), Sauti Soul (Kenya), Lij Mic (Ethiopia), pamoja na Rayvanny kutoka Tanzania.

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa kuamkia leo Nov 22, mwaka 2021 katika hotel ya Eko, huko nchini Nigeria.

Simulizi: Bado kidogo nipoteze mume baada ya kujifungua kwa upasuaji
Dj Sinyorita aibeba Tanzania tuzo za Afrima.