Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Eden Hazard ameanza kuipa presha timu yake ya Chelsea baada ya kugusua juu ya kuondoka klabuni hapo.

Hazard amekuwa akiwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid pamoja na PSG.

Real Madrid wamewahi kuonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo raia wa Ubelgiji, kwa dalili zinazoonekana wanaweza kuongeza presha ya kumuwania ikiwa ikiwa hatakuwa na furaha klabuni kwake.

Paris Saint-Germain maarufu kwa jina la PSG nao wamekuwa katika mikakati ya kuboresha kikosi chao na jina la mchezaji huyo limetajwa mara kadhaa.

Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni, Hazard amenukuliwa akisema: “Bado nina miaka miwili katika mkataba wangu wa sasa, najihisi vizuri kuwa hapa, mashabiki wananipenda, familia inafurahia lakini lolote linaweza kutokea, tusubiri tuone.”

Wachezaji tisa walamba kadi nyekundu
Familia yagoma kuupokea mwili wa marehemu Akwilina