Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania Eden Michael Walter Hazard, rasmi ametangaza kustaafu kuchezea Timu ya Taifa ya Ubelgiji.

Hazard ametangaza uamuzi huo, ikiwa ni siku chache baada ya Kikosi cha Ubelgiji kutolewa katika Fainali za Kombe la Dunia, Hatua ya Makundi.

Kiungo huyo amesema kuwa ni muda wake kutangaza maamuzi ya kustaafu, kwa sababu anaamini damu changa inahitajika kuendelea kufanya makubwa zaidi kwa ajili ya taifa lake la Ubelgiji.

Amesema amefanikisha sehemu yake katika Timu hiyo, lakini ana imani watakaokuja badala yake atafanya kazi kubwa ambayo itaiheshimisha zaidi Ubelgiji katika Michuano ya Kimataifa.

“Ninaamini muda wangu wa kuitumikia Timu ya Taifa umefikia kikomo, ni muda wa kuwapisha wengine ili waendeleze pale nilipoachia mimi, ninaamini vijana watakaokuja baadae wataiheshimisha nchi yangu.”

“Inauma kufanya maamuzi haya lakini sina budi kwa sababu mwisho umefika, ninawashukuru wale wote waliokua nami katika kipindi chote nilichoitumikia Timu ya Taifa ya Ubelgiji, ninawatakia kila la kheri kwa sababu ninajua asilimia kubwa wataendelea kulipambania taifa langu.” amesema Hazard

Hadi ametangaza kustaafu kuitumikia Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Hazard amecheza michezo 126 na kufinga mabao 33.

Kwa mara ya Kwanza Hazard aliitwa kuitumikia Timu ya taifa ya Wakubwa ya Ubelgiji mwaka 2008, huku akishiriki Fainali za Ulaya ‘Euro 2016 na 2020’.

Hazard ameshiriki Fainali mbili za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2020.

Wasanii wahamasishaji matumizi Dawa za kulevya waonywa
Kesi ya Bin Salman mauaji ya Khashoggi yafutwa