Kiungo wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Real Madrid Luka Modric anaendelea kupewa nafasi ya kuwika katika kinyang’anyiro cha tuzo mwaka huu, baada ya kufanya hivyo wakati wa fainali za kombe la dunia (Mchezaji bora wa fainali za kombe la dunia 2018), mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Ulaya na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA 2018.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Chelsea ya England Eden Hazard, ambaye ni miongoni mwa mchezaji wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2018, ametoa nafasi kwa Modric, kwa kusema anastahili kutangazwa mshindi.

Hazard, amesema kimtazamo Modric mwenye umri wa miaka 33, amefanya mambo makubwa msimu wa 2017/18, hatua ambayo ilimfanya kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa wa barani Ulaya mara tatu mfululizo na kuifikisha Croatia katika hatua ya fainali ya kombe la dunia.

“Anastahili, binafsi sioni mpinzani wa Modric katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or mwaka huu,”

“Wakati mwingine unapaswa kutoa nafasi kwa anaestahili, kwangu naamini Modric anastahili tuzo hii, baada ya kufanya vyema katika tuzo nyingine zilizotangulia mwaka huu.”

“Ninakiri siwezi kupambanishwa na Modric na uwepo wangu katika orodha ya wanaowani tuzo ya Ballon d’Or ni shemu ya taratibu tu, lakini ukweli ni kwamba huyu jamaa anajua na anapaswa kutangazwa mshindi.” Alisema Hazard.

Mwanzoni mwa mjuma hili waratibu wa tuzo za Ballon d’Or walitoa orodha ya wachezaji 30 wanaowani tuzo hiyo ambayo ilijuuisha majina ya mastaa wanaocheza soka barani Ulaya.

Orodha kamili ya wachezaji 30 waliotajwa kuingia katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or mwaka huu.

 

  1. Sergio Aguero (Manchester City, Argentina)
  2. Alisson (Liverpool, Brazil)
  3. Gareth Bale (Real Madrid, Wales)
  4. Karim Benzema (Real Madrid, France)
  5. Edinson Cavani (Paris Saint-Germain, Uruguay)
  6. Thibaut Courtois (Real Madrid, Belgium)
  7. Cristiano Ronaldo (Juventus, Portugal)
  8. Kevin De Bruyne (Manchester City, Belgium)
  9. Roberto Firmino (Liverpool, Brazil)
  10. Diego Godin (Atletico Madrid, Uruguay)
  11. Antoine Griezmann (Atletico Madrid, France)
  12. Eden Hazard (Chelsea, Belgium)
  13. Isco (Real Madrid, Spain)
  14. Harry Kane (Tottenham, England)
  15. N’Golo Kante (Chelsea, France)
  16. Hugo Lloris (Tottenham, France)
  17. Mario Mandzukic (Juventus, Croatia)
  18. Sadio Mane (Liverpool, Senegal)
  19. Marcelo (Real Madrid, Brazil)
  20. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain, France)
  21. Lionel Messi (Barcelona, Argentina)
  22. Luka Modric (Real Madrid, Croatia)
  23. Neymar (Paris Saint-Germain, Brazil)
  24. Jan Oblak (Atletico Madrid, Slovenia)
  25. Paul Pogba (Manchester United, France)
  26. Ivan Rakitic (Barcelona, Croatia)
  27. Sergio Ramos (Real Madrid, Spain)
  28. Mohamed Salah (Liverpool, Egypt)
  29. Luis Suarez (Barcelona, Uruguay)
  30. Raphael Varane (Real Madrid, France)

Riyama azamia kwenye muziki, 'Wimbo umetoka na unapendwa'
31 wafa poromoko la matope