Rais wa Zambia, Edgar Lungu amesema kuwa nchi za Kiafrika zinatakiwa kushirikiana ili kuweza kujikwamua na ushawishi wa ukoloni mambo leo kutoka nchi za kigeni.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea jumba la makumbusho ya mauaji ya halaiki yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

“Watu wote waliohusika kwenye mauaji ya kimbari popote wanafahamika nadhani kinachofuatia sasa ni kutazama makubaliano ya kisheria yaliyoko baina ya Rwanda na Zambia na kuangalia uwezekano wa kuharakisha utekelezwaji wa makubaliano hayo,”amesema Rais Lungu

Aidha, amesema kuwa Zambia haitakiwi kuwahifadhi watu hao na wala haitakubali kuwahifadhi wavunjaji wa sheria hivyo ni lazima wakamakatwe na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria kujibu unyama walioutenda.

Hata hivyo, Rais Lungu amesema matatizo ya nchi za Kiafrika kwa kiasi kikubwa yamekuwa na uhusiano wa mabaki ya ushawishi wa nchi za kigeni ambazo zilileta ukoloni kwa waafrika, hivyo mpaka sasa nchi hizo bado zinaonyesha ushawishi na kuwagawa waafrika kwa misingi ya ukabila, huku akitoa mfano wa nchi yake Zambia.

Video: Makonda amuweka kitimoto Mkurugenzi Temeke
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 22, 2018