Edinson Cavani amefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 ambao PSG imeupata katika michuano ya klabu bingwa dhidi ya Celtic na kuvunja rekodi ya Zlatan Ibrahimovic aliyekuwa akiongoza kwa kufunga mabao mengi katika klabu ya Paris Saint-Germain kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Ibrahimovic alikuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kufunga mabao 20 lakini sasa Cavanni anakuwa na mabao 22 baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Celtic na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa PSG katika michuano ya Ulaya.

Mabao mengine ya  Paris Saint-Germain yalifungwa na Neymar ambaye ndiye aliyetangulia kufunga bao la kwaza dakika ya 19 wakati Kylian Mbappe akifunga bao lingine dakika ya 57.

Mabao hayo na lile la kujifunga la Mikael Lustig liliwafanga PSG kuibuka kidedea na ushindi wa bao 5 kwa bila ugenini dhidi ya Celtic.

Cavani anacheza katika kikosa cha PSG kinachonolewa na kocha Unai Emery ikiwa ni msimu wake wa nne tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2013 akitokea katika klabu ya Napoli.

 

Hector Bellerin avipinga vyombo vya habari
Marekani itajuta kama itaendelea kutuchokoza: Korea Kaskazini