Baada ya taarifa kusambaa kuwa aliyekuwa Kocha wa Yanga Princess na ambaye kwa Sasa ni Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake Edna Lema kupokea ofa nono kutoka kwa Boss wa Oysterbay Queens, Kocha huyo amesema Watanzania watulize mzuka kwani mambo mazuri zaidi yanakuja.

Edna amesema, sio ofa hiyo tu ambayo amepokea lakini kwa swala la maamuzi bado ajafanya hivyo Mashabiki wawe na subila.

“Ni kweli nimepokea ofa hiyo, lakini sio hiyo tu ambayo ninayo mkononi, zipo nyingi lakini hakuna ambao nimewapa majibu ya kukubali kwasababu ninahitaji kupumzika msimu huu” amesema Edna Lema.

Edna msimu uliopita aliisaidia Yanga Princess kushika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania bara baada ya kuachwa point moja tu na Mabingwa Simba Queens.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 3, 2021
TMA: Mvua za Vuli kuanza