Mchambuzi nguli wa soka nchini, Edo Kumwembe ameweka wazi kuwa timu anayoipa nafasi ya kushinda pambano la watani wa Jadi ni Simba, kutokana na aina ya wachezaji alionao msimu huu.

Edo amesema kuwa nafasi kubwa ipo kwa Simba. huku akiielezea timu hiyo kuwa imekuwa bora zaidi msimu huu ukizingatia haijapoteza mchezo hata mmoja.

”Mimi nawapa Simba ‘Advantage’ ya kushinda pambano la leo kutokana na wachezaji wao watatu Okwi, Kichuya na Bocco ambao wako kwenye kiwango cha juu zaidi msimu huu hivyo wanaweza kuamua matokeo ya ushindi wa Simba,” amesema Edo

Aidha, amesema pamoja na Simba kuwa na nafasi kubwa lakini wasisahau mpira unadunda. na ameongeza kuwa hata misimu kadhaa Yanga amewahi kuwa kwenye ubora lakini Simba walishinda kwa hiyo lolote linaweza kutokea.

Hata hivyo, timu zote mbili zilikuwa zimeweka kambi mkoani Morogoro kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao umevuta hisia za mashabiki kwani mchezo huo ndio utakao amua nani atakwenda kutwaa kombe.

Video: Askofu Malasusa aipasua KKKT, Utata kodi ya mafuta ghafi kuchochea bei
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 29, 2018

Comments

comments