Rapa Edu Boy amemtaka mkali wa mistari konde ambaye ni mwanafamilia wa ‘Rostam’, Stamina kuacha kumtafuta mitaani bali wapande ulingoni kwa pambano litakalowaingizia pesa.

Rapa huyo ambaye amekuwa akitoa nyimbo zenye mistari tata dhidi ya wasanii wenzake, hivi karibuni ameachia ‘Tunasafisha’ ambayo ndani yake pia amemkwaruza Stamina.

Kulikuwa na tetesi kuwa Stamina anamtafuta mtaani ili amfunze adabu, lakini rapa huyo amesema ana uhakika hawezi kumpiga mtaani kwakuwa kuna sheria.

“Najua Stamina hawezi kunipiga mimi. Si kuna sheria. Lakini tuache hizi habari za kusakana mtaani, kama vipi twende pale leaders tutangaze pambano ‘mtu mbili’, tuingize na mpunga,” alisema Edu Boy.

 

Katika hatua nyingine, Edu Boy alisema kuwa amefungua studio yake jijini Mwanza anakotoka kwa lengo la kuwasaidia wasanii wengine wa Mwanza.

Prezzo afunguka kutompost Amber Lulu kwenye ‘birthday’ yake
Makunga abwaga manyanga, ajiuzulu