Meneja wa klabu ya Sevilla CF Eduardo Berizzo atafanyiwa upasuaji leo Jumanne baada ya kupatikana na saratani ya tezi dume mapema mwezi huu.

Hali ya mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 ilitangazwa baada ya kikosi chake kutoka nyuma na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool katika kombe la vilabu bingwa wiki iliopita.

uongozi wa klabu ya Sevilla umesema  kurudi kwa Berizzo kutategemea muda atakaochukua kupona upasuaji huo.

Naibu mkufunzi wake Ernesto Marcucci ataiongoza timu hiyo kwa sasa.

Berizzo aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Sevilla msimu huu kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya kuifunza Celta vigo kwa takriban miaka mitatu.

Wenger: Sanchez, Ozil hawaondoki Januari
BREAKING: Hali yawa tete Kenya, Uhuru akiapiswa