Kwa kipindi cha mwezi sasa waislamu walikuwa katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakitimiza ya ibada ya nguzo za uislamu ambayo ni Kufunga.

Baadhi ya waislamu kutoka mataifa mbali mbali  wakiwepo wajerumani na afrika magharibi Naijeria, leo wamesherekea sikukuu ya Eid Ul fitr baada ya kumaliza funga zao.

Hata hivyo leo Mufti Mkuu wa tanzania Zubeir Bin Ally amewataka  pia waislam kujitokeza  kesho katika misikiti mbalimbali kwa ajili ya ibada ya Eid ul Fitr.

Taarifa ambayo imetolewa  muda mfupi uliopita ni uthibitisho wa  sikukuu ya Eid ul Fitr ambapo Waislam wote walikua wakisubiri kuandama kwa mwezi.

Kwenye taarifa yake Muft Zubeir amesema Mwezi huo umeonekana sehemu mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania.

 

Video: Ajali 3 zilizosababisha vifo vya watu 46, majeruhi 75 chanzo ni uzembe wa Madereva
Wamiliki wa Magari Watahadharishwa na Utapeli Dar.