Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Young Africans hali kadhalika Mchezaji Hassan Hamisi Ramadhani maarufu kama Hassan Kessy, Wakili Msomi, Mzee Said El-Maamry anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa madai hayo.

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliagiza pande za Simba na Young Africans kumaliza suala hilo mapema mwezi uliopita, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake walishindwa kufanya hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka huu.

Hata hivyo, msuluhishi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka Young Africans kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa safarini Iringa alikokwenda kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.

Ilielezwa kuwa Mgongolwa ambaye ni Mwanasheria wa Young Africans, alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine.

Kutokana na hali hiyo, E-Maamry amepanga sasa kukutana nna viongozi / Wawakilishi wa pande zote mbili Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia namna ya kumaliza madai ya Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni dhidi ya Young Africans ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.

Mzee El-Maamry amesema: “Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikilizwa. Ni vema Mwanasheria wa Young Africans akasubiriwa.”

Kamati ya TFF inasuburi makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye Kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza soka.

Wajumbe Wa Kamati Ya Utendaji TFF Wampongeza Rais Malinzi
Lukaku Awapotezea Viongozi Wa Everton