Aliyekuwa mshambuliaji nyota wa Stand United, Elias Maguli amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Dhofar SC ya nchini Oman.

Maguri ambaye alionyesha kiwango cha juu msimu uliopita kabla hajaanza kutoelewana na uongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, alisaini mkataba huo jana.

Klabu hiyo ndiyo wawakilishi wa Oman katika michuano ya Bara la Asia, hivyo hii itampa Maguli nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa zaidi.

Awali alikuwa akiwindwa na timu kadhaa ikiwemo Simba ya jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kujiunga nazo na kutimkia nchini Oman.

Kabla ya kwenda kwenye timu hiyo, Maguri ambaye alitoka Simba kabla ya kujiunga na Stand aliwahi kufanya majaribio kwenye timu ya TP Mazembe na kusema kuwa amefanikiwa kufuzu, ingawa klabu yake ilimgomea  kwa kuwa hakufuata utaratibu wakati wa kwenda kwenye majaribio hayo.

Msimu uliopita mshambuliaji wa huyo wa Taifa Stars, aliifungia timu yake mabao 15 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Amissi Tambwe (21), na Donald Ngoma (17).

Kipaji Ndumba Kunanii Diamond Platnumz!!
Majaliwa Kumuwakilisha Magufuli Kesho Botwasana