Mshambuliaji wa Tanzania Elias Maguri ametumia sehemu ya maisha yake kisoka kuandika na kutuma ujumbe kwa mashabiki na wachezaji wanaochipukia, ili kutoa somo la kimaisha.

Maguri alianza kutamba katika soka la Tanzania akiwa na klabu ya Prisons FC mwaka 2013 kicha alisajiliwa na Ruvu Shooting mwaka 2014, na ndipo Simba SC walipomuona na kumuhamishia Msimbazi mwaka 2015.

Mwaka mmoja baadae mzaliwa huyo wa mjini Musoma mkoani Mara, akatimkia Stand United na kisha akatimiza ndoto za kucheza soka nje ya nchi baada ya kusajiliwa na klabu ya Dhofar ya nchini Oman mwaka 2018.

Mwaka 2019 alirejea barani Afrika na kutua mjini Kigali, Rwanda baada ya kusajiliwa na klabu ya AS Kigali, kabla ya kurudi nyumbani Tanzania kujiunga na KMC FC mwezi Agosti mwaka huo.

Mwezi Machi mwaka huu aliondoka na kuelekea Zambia kujiunga na klabu ya Nak. Leopards, kisha akaondoka na kutimikia FC Platinum ya Zimbabwe miezi kadhaa iliyopita.

Huenda kupanda na kushuka kwa soka lake kukawa kumemfanya apate ujasiri wa kuandia ujumbe alioupa jina la USIOGOPE KUANZA UPYA, wenye vipengele vitano.

ANDIKO LA MAGURI LINAANZIA HAPA:

Moja ya mtihani mkubwa ambao utakutana nao kwenye maisha yako ni kuanza upya.

Hili ni jambo wakati mwingine unajikuta mazingira ya kutokea unalazimika kuanza upya,mfano Kuna watu ambao walikua katika ofisi wanafanyakazi na wakiamini watazeekea hapo, lakini kuna mambo yakaharibika na kusababisha kuanza upya.

Wakati mwingine kuanza upya kunasababishwa na changamoto lakini wakati mwingine kunaweza kusababishwa na fursa mpya ambayo umeipata ni nzuri zaidi kuliko uliyonayosaizi.

Ndio Maana kila wakati unapotaka kuanza upya huwa kuna hisia mbili ambazo husababisha kufikiria vitu tofauti kabla ya kuchukua uamuzi,

*(1) Hofu_hutokea Maana hujui yajayo

*(2)furaha_hii unajua kuna ukurasa mpya unaufungua.

Wakati mwingine kuanza upya usikuepuke,lakini ni Kuna mambo ya msingi ambayo ni Muhimu sana kuyajua kila wakati unapotaka kuanza upya.

(1)Bora uanze upya kuliko muelekeo sio

Wengine wanajua kabisaa mahali au wanachofanya sio sahihi lkn wanaona ni bora waendelee kuliko upya,hii ni mbaya sana kwani itakugharimu badae.., Gharama utakayoitumia kuanza upya ni ndogo kuliko gharama utakayoitumia kujutia mwisho wa siku kufanya kitu kisichokua sahihi.

(2)Kuanza upya sio ngumu kama unavyofikria

Mabadiliko ni sehemu ya kitu kinachokusaidia kwenda mbele, Maana kuna wengine wamekua na fikra potofu kuwa hawawezi kufanya chochote pasipo mtu fulani,ama wakiondoka katika ofisi fulani hawatoweza kufanya chochote

(3)Unavyochelewa kuanza upya,unachelewa mafanikio

Watu wengi wamekua na tabia ya kusema nitafanya kesho jambo linalowezekana leo, kadri Unavyochelewa ndivyo gharama huongezeka

Mwingine anaweza kusema ngoja nijipange kwanza Maana nitaumia kumbe badae atatakiwa kujipanga zaidi kuliko ambavyo ungeanza sasa.

(4)Anza kidogo kidogo

Kama huwezi kufanya kitu kikubwa,fanya kidogo kwa namna kubwa,hapa kuna wengine wanaogopa kuanza kidogo pengine waliwahi kuwa na majina makubwa au kuwa mabosi sehemu, wanaogopa jamii itawachukulia vipi

Kumbe unatakiwa kujenga kidogo kwa mda mrefu kadri unavyoweza kuweka msingi.

(5)Sikiliza ndani yako

Watu wengi hawapendi kusikiliza ndani yao bali hupenda kusikiliza watu wengine,hawa wanaendeshwa na maoni ya watu wengine,..Usipojitambua wewe ni nani basi dunia itakufanya vile itakavyo

Matarajio ya watu wengine yasikufanye kushindwa kuanza upya,…Kuanza upya hakumaanishi umefeli bali umejitambua na uko tayari kitu kipya kwenye maisha yako.

BREAKING: JPM aagiza vyuo, kidato cha sita, michezo, utalii kufunguliwa
Nchimbi: Kipigo cha Kagera Sugar kiliniuma