Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA).

Amesema kuwa ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa.

Ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Parokia ya Ikwiriri, mkoani Pwani. ambapo ameipongeza Parokia hiyo kwa kubuni mradi wa ujenzi wa shule.

Amesema sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi na wadau muhimu wa sekta hiyo ni pamoja na Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya kiraia na ya kidini, sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

”Hivi sasa kila Kijiji nchini kina shule ya msingi na ongezeko limefikia idadi ya shule 17,659 zikiwemo zilizo chini ya Kanisa katoliki 204. Pia tumeweza kujenga shule za sekondari katika kila kata ambapo ongezeko limefikia shule za sekondari 4,883 nchi nzima zikiwemo zilizo chini ya kanisa katoliki 266,”amesema Majaliwa

Aidha, katika hatua nyingine, Majaliwa amesema lengo la Serikali kutoa Elimu msingi bila Ada ni kuleta ujumuishi kwa kuhakikisha watoto wote hususani wale ambao wanatoka katika familia zisizo na uwezo wanapata haki ya msingi ya kupata elimu.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametumia fursa hiyo kuishikuru Serikalikwa kurejesha hali ya usalama na utulivu katika eneo la Rufiji na Kibiti.

 

Rick Ross kamkingia kifua 'Cardi B' skendo ya kulevya na kutapeli wanaume
Bunge la Uingereza kupiga kura kwa mara ya tatu