Serikali imesema kuwa mpango wa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne umeanza rasmi leo nchi nzima.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ameuambia umma wa watanzania kuwa tayari serikali imeshapeleka fedha kwa ajili ya kugharamia elimu hiyo katika kila shule nchini.

Katika hatua nyingi, serikali wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga imetangaza kuwasaka na kuwachukulia hatua kali watu wanaowashawishi na kuwapa ujauzito wanafunzi katika wilaya hiyo, hali inayorudisha nyuma juhudi za wazazi katika kuwapa elimu watoto wa kike.

Akiongea leo wilayani humo baada ya kusikiliza malalamiko ya wazazi, Mkuu wa wilaya hiyo, Bi.Hawa Ng’humbi alitoa onyo kali kwa watu wanaowarubuni wanafunzi na kuwakatiza masomo yao, huku akiwasisitiza wazazi kuhakikisha wanawapa watoto wao wa kile elimu kadri inavyowezekana.

 

Dakika 180 Za Vita Azam FC Ligi Kuu
Mshindi Wa Tuzo Ya Dunia Kujulikana Leo