Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Freddie Ljungberg ameteuliwa kuwa Kocha wa timu hiyo baada ya  Unai Emery kufutwa kazi baada ya kuongoza timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18.

Ljungberg ambaye amechukua nafasi Emery, awali alikuwa mkufunzi wa Paris St-Germain katika ligi ya Ufaransa na kushinda mataji matatu ya Ulaya akiwa na Sevilla, aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Arsenal mwezi Mei 2018, akimrithi Arsene Wenger.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Arsenal inasema kwamba uamuzi huo ulichukuliwa baada ya matokeo ya timu hiyo kushindwa kufikia kiwango kilichohitajika.

Arsenal haijashinda katika mechi saba na ilipoteza 2-1 nyumbani dhidi ya klabu ya Ujerumani Eitracht Frankfurt katika ligi ya Ulaya siku ya Alhamisi.

Arsenal ilianza msimu huu wakiwa na mfululizo wa ushindi dhidi ya Newcastle na Burnley, lakini ushindi huo ulimalizwa baada ya kulazwa na Liverpool, kabla ya kurekodi sare mbili dhidi ya wapinzani wao wa London Tottenham na Watford.

Siku ya Jumamosi, walitoka sare ya 2-2 ikiwa ni ya sita msimu huu nyumbani dhidi ya Southampton, huku Alexander Lacazette akifunga goli la kusawazisha katika muda wa majeraha.

Emery ni mkufunzi wa tatu kufutwa kazi katika ligi ya England msimu huu baada ya Javi Gracia na Mauricio Pochettino.

Ushindi wa mwisho wa Arsenal ulijiri dhidi ya Vitoria Guimaraes katika ligi ya Yuropa tarehe 24 mwezi Oktoba , ambapo walihitaji mipira miwili ya adhabu kupata ushindi wa magoli 3-2.

Ljungberg ameanza kuiongoza katika mazoezi timu hiyo na taarifa ya Arsenal ilisema wana matumaini na Freddie Ljunberg kuwaogoza. Usakaji wa kocha mpya unaendelea na watatoa tangazo tutakapokamilisha mpango huo.

Majina mengine yanayohusishwa na tangazo hilo ni pamoja na mkufunzi wa zamani wa Tottenham, Pochettino naibu kocha wa Manchester City Mikel Arteta, mkufunzi wa zamani wa Juventus Massimiliano Alegri na Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe.

Walianza msimu huu kwakutoa zaidi ya £130 milioni walipomsaini winga Nicolas Pepe, beki wa katikati David Luiz, Beki wa kushoto Kieran Tierney, mshambuliaji Gabriel Martinelli na beki William Saliba, ambaye atajiunga msimu ujao.

Pia klabu hiyo ilimununua kwa mkopo kiungo wa kati Dani Ceballos kutoka Real Madrid.

Video:Mwakinyo ameshinda kwa haki? Promota, mashabiki, wafilipino wafunguka
IGP Sirro alivyokimbiwa na mchumba kisa Mzawa wa Mara