Nyota mwingine wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, Emmanuel Emenike ametangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo.

Emenike, mwenye umri wa miaka 28, ametangaza hayo siku chache tu, baada ya mlinda mlango wa klabu ya Lille ya nchini Ufaransa Vincent Enyeama kutangaza kujiweka pembeni.

Wachezaji hao wawili wametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kutangaza maamuzi yao ya kustaafu soka upande wa timu ya taifa ya Nigeria, hatua ambayo imechukuliwa kama sehemu ya kuwafikishia habari mashabiki wao kwa uharaka zaidi.

Eminike alinukuliwa na gazeti la Premium Times la nchini kwao Nigeria, akisema imekuwa furaha kubwa sana kwake kuichezea timu ya taifa, huku akisisitiza kutokujutia hali hiyo kutokana na maisha mazuri aliyokua akiishi na wachezaji wengine ambao mara kadhaa alikutana nao kikosini.

Eminike, alitumika nafasi hiyo ya kuzungumza na chombo hicho cha habari kuwashukuru mashabiki ambao walimuunga mkono katika kipindi chote ambacho aliitumikia timu ya taifa ya Nigeria, huku akiwataka kumsamehe kwa mabaya aliyoyatenda na kudumisha mapenzi waliyonayo dhidi yake.

Hata hivyo habari ya kustaafu Eminiek, zimepokelewa kwa hisia totauti miongoni mwa mashabiki wa soka nchini humo, ambapo baadhi yao wanaamini huenda kuna  maelewano mabaya kati yake na kocha wa sasa, Sunday Oliseh.

Emenike ameitumikia timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) katika michezo 35 na kufunga mabao 6.

Alikuwa mfungaji wa mabao bora katika fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2013.

Mwisho Wa Ubaya Aibu, Madudu Yabainika FIFA
Maalim Seif Amtega Dkt. Shein Matokeo ya Urais