Msanii wa injili ambaye aliwahi kuwa mume wa Flora, Emmanuel Mbasha amemshukuru Flora kwa kumzalia mtoto wa kike mzuri lakini pia ametumia nafasi hiyo kutoa malalamiko yake kubaniwa kuonana na mtoto wake huyo kwa muda wa miaka miwili.

Ameyasema hayo kupitia mitandao ya kijamii kufikisha kilio chake kwa mzazi mwenzie huyo ambaye sasa ameolewa na Daudi Kusekwa na kumtaka japo kumpa haki yake ya kuonana na mtoto wake huyo ambaye anadai kuwa amemlea toka akiwa mdogo.

“Ulinizalia mtoto mzuri sana kwa hilo nakushukuru mno. Nimemmiss Lizy sana unipe basi mtoto unaninyima kabisa daah karibu mwaka wa 2 inaelekea wa 3 sasa sijamwona mtoto du mimi baba yake tu, ila nakuomba hata siku moja moja nifurahie maisha na dogo basi, nakuomba nimwone mwanangu Lizy. Najua hata mtoto amenimiss sana mana ameondoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tangu mtoto ila anashindwa kuongea tu, ila najua ananikumbuka sana,”amesema Mbasha.

Amesema kuwa anachofanya Flora ni kwenda kinyume na sheria na kupingana na amri ya mahakama ambayo ilimpa nafasi kama mzazi kumuona mtoto wake.

Hata hivyo, mahakama iliamua mtoto akae na Mama yake lakini baba mzazi awe na nafasi ya kuweza kuonana na mtoto pindi anapohitaji.

 

Video: Mtu mrefu kuliko wote jijini Dar afunguka, awataka watu wasimshangae
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 11, 2018