Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amezungumzia uwezekano wa kurudiana na mkewe Flora ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu walipotengana na kukabiliwa na misukosuko ya kesi ya kumbaka shemeji yake ambayo hata hivyo aliishinda.

Emmanuel alitengana na mkewe baada ya kumshtumu kwa kumsaliti huku mwanamke huyo pia akimrushia tuhuma nyingi nzito ikiwa ni pamoja na ile ya kumbaka shemeji yake.

Hata hivyo, upepo ulitulia na wawili hao walionekana kila mmoja akijaribu kufanya kazi zake, ambapo hivi karibuni Emmanuel ametambulisha ujio wa albam yake mpya ya njimbo za injili.

Akizungumzia uwezekano wa ndoa hiyo kurejea, Mbasha amedai kuwa hilo liko mikononi mwa Flora ambaye aliandaa mazingira ya kuachana, lakini akasisitiza kuwa itakuwa ngumu.

“Mimi kurudiana na Flora Mbasha ni ngumu kwasababu yeye ndio aliniacha mimi na yeye ndio aliandaa mazingira yake ya kuniacha mimi mpaka ikafika wakati Familia yangu, viongozi mbalimbali wa Dini wakawa wanamshauri lakini akutaka kurudiana na mimi kwahiyo naweza sema ni ngumu kurudiana na Flora,” alisema Mbasha.

Akihojiwa hivi karibuni na Friday Night Live ya East Africa TV, Emmanuel Mbasha alisisitiza kuwa hadi leo yuko ‘single’.

Riyad Mahrez Afunga Mjadala, Ajitia Kitanzi Hadi 2020
TCRA kuwashughulikia wanaotumia majina ‘feki’ mitandaoni