Eneo la ardhi lililokuwa limetengwa kwa ajili ya kujengwa Ikulu ndogo ya mkoa wa Mbeya limedaiwa kuuzwa kinyamela na maofisa ardhi wa mkoa huo.

Hayo yalibainika jana baada ya Mkoa wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala kufanya ziara katika eneo hilo lililoko katika eneo la chuo cha VETA ambapo alishuhudia majengo ya makazi yaliyojengwa katika eneo hilo kinyume cha taratibu.

Maafisa ardhi hao wanadaiwa kula njama na kupima viwanja hivyo wakiwagawia wananchi ambao walitakiwa kujiweka kwenye nafasi ya umiliki na kuonekana wao ndio waliowauzia watu waliojenga eneo hilo.

Akifafanua sakata hilo, Diwani wa kata ya Ilomba, Dickson Mwakilasa alimwambia Mkuu wa mkoa huo kuwa eneo hilo ni la Serikali na kwamba kilichoakiwa ni kuwalipa fidia watu waliokuwa na mashamba ndani ya eneo hilo lakini imefanyika vinginevyo.

Baada ya kuwahoji maofisa ardhi ambao walionekana kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu historia ya eneo hilo, Makalla aliahidi kufuatilia nyaraka na kulitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Bilic: Diego Costa Alistahili Kadi Nyekundu
Kubenea ajisalimisha Polisi kwa uchochezi