Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba SC yamekamilika, na wana kila sababu ya kushinda mchezo huo ili kutinga Fainali Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC).

Hersi alikua na kikosi cha Young Africans huko Bukoba akisimamia masuala muhimu kuelekea mchezo huo, unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

Amesema Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC) ndio nafasi pekee kwao kuweza kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Lakini pia, amesema GSM kama moja ya wadhamini hawako tayari kuona Young Africans inakwenda msimu wa tatu bila kushinda taji lolote.

“Ni aibu kwa timu kubwa kama Yanga katika ukanda huu wa Afrika kushindwa kuchukua kombe, hivyo kama wadhamini tumepanga kufuta aibu hiyo kwa kuhakikisha tunafanya kila liwezekano lililokuwepo ndani ya uwezo wetu ili tuchukue ubingwa huu”

“Tumeandaa kambi nzuri na bonasi za wachezaji kuelekea mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Simba, lengo ni kuwaongezea morali wachezaji ya kupambana ili malengo yetu ya kuchukua kombe hilo yatimie”

Kama ilivyokuwa mchezo wa March 08, wachezaji wa Young Africans ‘watasepa’ na Mamilioni kama wataifunga Simba SC na kutinga fainali ya michuano ya kombe la FA ambayo bingwa wake atakwenda kupatikana mkoani Rukwa.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Simba SC, GSM walitoa bonus ya Shilingi Milioni 200, inaelezwa fedha walizoahidiwa wachezaji kama watashinda Jumapili  ni zaidi ya kitita hicho.

Sita kuamua Simba Vs Young Africans
Mashabiki 30,000 kushuhudia Simba SC Vs Young Africans

Comments

comments