Timu ya taifa ya England itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hispania katika uwanja wa Wembley Novemba 15.

Kocha mkuu wa timu hiyo Sam Allardyce, atautumia mchezo huo kama sehemu ya kukiandaa kikosi chake ikiwa ni siku chache baada ya kupambana na Scotland katika mpambano wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

England wanaamini mabingwa hao wa dunia mwaka 2010 watakua kipimo kizuri kwao katika kipindi ambacho watahitaji kuona mapungufu ambayo yatamuwezesha kocha Allardyce kujipanga vyema kabla ya kuendelea na kampeni za kusaka tiketi ya kuelekea nchini Urusi mwaka 2018.

England na Hispania zote zilishindwa kutimiza malengo ya kufanya vyema kwenye fainali za Euro 2016, baada ya kuenguliwa kwenye hatua ya 16 bora.

Kwa mara ya mwisho mataifa hayo yalikutana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa mwezi Novemba mwaka 2015, na Hispania walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Man Utd, Chelsea Zakabana Koo Kwa Wabrazil
David Alaba Aipotezea Real Madrid