Klabu ya West Bromwich Albion, imedhamiria kuwasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya West Ham United, Enner Valencia.

Valencia, hakuwa na muendelezo mzuri wa soka lake kwa msimu wa 2015-16, kufuatia majareha yaliyokua yakimkabili mara kwa mara, hatua ambayo ilipelekea apoteze nafasi katika kikosi cha kwanza cha wagonga nyundo hao wa jijini London.

Uongozi wa West Bromwich Albion, unaamini mshambuliaji huyo kutoka  nchini Ecuador, atawafaa kwa msimu ujao wa ligi ya nchini England, hasa baada ya kuwaachia Victor Anichebe pamoja na Stephane Sessegnon mwanzoni mwa juma hili, kwa kuwapa ruhusa ya kusaka klabu nyingine.

Valencia, alisajiliwa na West Ham Utd, baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil, ambapo alionyesha uwezo mkubwa akiwa na timu yake ya taifa.

Akiwa West Ham Utd, Valencia mpaka sasa ameshafanikiwa kucheza michezo 48 na kufunga mabao manane.

Wageni Watesa Ligi Ya Soka Marekani (MLS)
Van Gaal Aombwa Kuwa Bosi Wa Jose Mourinho