Licha ya kuwa na kibarua cha kuinoa timu ya Taifa ya Hispania hadi 2022, aliyekua meneja wa klabu za AS Roma (italia), Celta Vigo pamoja na Barcelona (zote za Hispania) Luis Enrique, amesema yupo tayari kuifundisha klabu yoyote ambayo aliwahi kuitumikia siku za nyuma.

Enrique aliweka bayana mpango huo wa kuwa tayari kurejea kwenye klabu hizo, alipoulizwa katika kipindi cha maswali na majibu (Q&A) kutoka kwa Mashabiki kwamba ni klabu gani ambayo unaweza kuinoa tena na kujibu… ” Klabu yoyote ambayo niliwahi kuinoa hapo awali “.

Kocha huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 49 aliongeza kwa kusema.. ” Siku zote milango ipo wazi kwa vilabu vyote ambavyo niliwahi kuvinoa hapo awali, nilikuwa na wakati mzuri sana na Barcelona na Siku zote nitakuwa hivyo kwao “.

Akiwa kocha wa Barcelona, Luis Enrique alifanikiwa kutwaa mataji 9 kati ya mwaka 20014 na 2017 likiwemo taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya Ligi kuu ya Hispania na matatu ya Kombe la Mfalme.

Sababu kubwa ya Enrique kuachana na Barcelona ni kutokana na matatizo mbalimbali ya kifamilia hasa kuhusu Binti yake ambaye alikuwa anaumwa kabla ya kupoteza maisha.

CoronaTanzania: Mgonjwa wa tatu amepona, hakuna kisa kipya
Watano mbaroni mauaji ya askari wa JWTZ