Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza kuitupa nje ya michuano ya klabu bingwa barani humo, klabu ya Entente Setif ya nchini Algeria, kufuatia ghasia zilizoonyeshwa na mashabiki wake wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini.

CAF, wamefuatilia mkasa huo na kujiridhisha kulikua na ghasia za makusudi zilizofanywa na mashabiki wa klabu ya Entente Setif, kwa kurusha vitu vyenye ncha kali, chupa za maji pamoja na miale ya moto katika sehemu ya kuchezea.

Kitendo hicho kilimlazimu muamuzi kusimamisha mchezo kwa muda, kwa kuzingatia hali ya usalama kwa wachezaji, maafisa wa klabu zote mbili pamoja na mashabiki wengine ambao walikua katika hali ya utulivu.

Hata hivyo maamuzi hayo yanaipokonya ushindi wa mabao mawili na point tatu klabu ya Mamelodi Sundowns ambayo ilijitutumua na kufanikiwa kuibuka na ushindi katika uwanja wa ugenini.

Bado klabu ya Entente Setif ina wigo mpana wa kukata rufaa ya kupinga maamuzi yaliyochukuliwa na CAF dhidi yao.

Rais Wa Paris St Germain Amfuta Kazi Laurent Blanc
Video: JPM: Nitamlinda JK, Wastaafu. Sasa UKIMWI kupimwa nyumba kwa nyumba - Magazeti leo Jun 24, 2016