Ligi kuu ya Soka ya England (EPL) imesimamishwa mpaka pale itakapokuwa salama kucheza tena , na pia wametangaza wachezaji huenda wakapunguzwa mshahara wao kwa asilimia 30 .

Taarifa kutoka tovuti yao imesema kwamba kuna hatua mpya zitachukuliwa baada ya kikao cha washika dau wa Ligi huyo kufanyika leo ambacho kimemalizika .

Taarifa inasema,” Kwanza kabisa imethibitishwa kipaumbele namba moja ni kulinda afya na uhai wa taifa pamoja na jamii yetu wakijumuishwa wachezaji, makocha , wafanyakazi wa vilabu na mashabiki . “

Imethibitishwa kwamba Ligi kuu ya Uingereza haitorudi mwezi Mei , kwamba msimu wa 2019/2020 utarejea hali ikiwa salama na sahihi kucheza Ligi .

Tarehe ambayo mechi zitaanza kuchezwa inafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara mpaka ipatikane.

Wakati huo huo Klabu za (EPL) zimekataa mpango wa kumalizia Ligi hiyo Nchini China, hii ni baada ya moja ya klabu zinazoshiriki katika Ligi hiyo ambayo haikutajwa jina, kupendekeza kumalizia mechi zilizosalia Nchini China.

Klabu za EPL zaomba kanuni ibadilishwe
Video: Corona yamfikisha Masanja Polisi