Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, katika hotuba yake kwa taifa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2023, alisifu ushindi wake kama ushindi wa demokrasia.

Akizungumza mbele ya mamia ya maelfu ya watu waliokusanyika katika ua wa jengo la rais mjini Ankara, Rais Erdogan alisisitiza umoja, na kutangaza kwamba washindi wa kweli wa duru ya pili ya uchaguzi wa Jumapili walikuwa raia milioni 85 wa Uturuki na demokrasia ya Uturuki.

“Uturuki ndiye mshindi, demokrasia yetu ndio mshindi, Hakuna aliyepoteza leo. Sisi wote milioni 85 tumeshinda. Sasa ni wakati wa kuungana kutimiza malengo yetu ya kitaifa na ndoto za kitaifa” amesema Erdogan.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Kuchaguliwa tena kwa Erdogan kulithibitishwa na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Uchaguzi nchini humo (YSK) Jumapili jioni.

Kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi, Ahmet Yener alisema Erdogan alishinda kwa asilimia 52.14, huku Kilicdaroglu akipata asilimia 47.86 ya kura, na kuongeza kuwa asilimia 99.43 ya masanduku ya kura yamefunguliwa hadi sasa.

Katika moja ya chaguzi muhimu zaidi katika historia ya vyama vingi vya siasa, taifa letu lilifanya uamuzi wake kwa ajili ya ‘Karne ya Uturuki’,” Erdogan alisema. ambapo aliongeza kuwa uchaguzi huu ulikuwa “muhimu zaidi” kwa Uturuki katika zama za kisasa.

“Tunapaswa kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya watu wetu,ili Kuponya majeraha ya tetemeko la ardhi la Februari 6 na kujenga upya miji iliyoharibiwa kutaendelea kuwa kipaumbele cha juu cha serikali ” alisema Erdogan.

Pia aliwakumbusha watu kwamba siku iliyofuata, Mei 29, inalingana na kumbukumbu ya kutekwa kwa Istanbul na Sultan Mehmet II wa Ottoman mnamo 1453.

“Ushindi wa Istanbul, ambao tutaadhimisha kesho katika kuadhimisha miaka 570, uliashiria mwanzo wa enzi mpya huku ukimaliza enzi ya zamani,” alisema Erdogan

Recep Tayyip Erdoğan na Kemal Kilicdaroglu

“Natumai wakati huu muhimu katika historia yetu ya Karne ya Uturuki ambayo tunaona chaguzi kama hizi itaacha alama yake.” Erdogan

Dickson Job: Tunajuwa mbinu zao wakiwa Algeria
Tinubu kuapishwa rasmi leo, Rais Samia awasili kushuhudia