Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Ufaransa, Eric Cantona anatarajiwa kurudi katika uwanja wa Old Trafford mwezi Juni.

Cantona anatarajia kushiriki katika kikosi cha wachezaji 11 maarufu kitakachoshirikisha wachezaji wa zamani na watu maarufu wakiongozwa na nahodha Usain Bolt. ambapo kwake itakuwa mara ya kwanza kwa yeye kucheza katika uwanja huo tangu 2001.

”Ninarudi kuhakikisha kuwa mechi hiyo ya Juni 10 ndio bora zaidi na nataka mujiunge nami, njooni tuungane tuweke historia katika uwanja wa Old Trafford kwa mara nyengine tena,”amesema Cantona

Aidha, Eric Cantona ataungana na wachezaji wengine wa zamani wa Manchester United akiwemo, Phil Nevile na Edwin van der Sar, wengine katika kikosi hicho cha dunia ambacho watapambana na wachezaji wa zamani wa Uingereza ni pamoja na Yaya Toure, Clarence Seedorf, Robert Pires , Jaap Stam na Patrick Kluivert.

Kwa upande wa kikosi cha zamani cha Uingereza kitakuwa wachezaji kama David Seaman, Jamie Redknapp, Danny Murphy na Robbie Fowler.

Hata hivyo, Cantona ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United kwa dau la £1.2m in 1992 – alifunga mabao 64 katika mechi 143 za ligi alizochezea Manchester United na kushinda mataji manne ya ligi ya Uingereza pamoja na mataji mawili ya kombe la FA katika misimu mitano.

 

Alikiba aipa tano 'Hapa Kazi tu' ya JPM
Hatuwezi kukaa na mawaziri hapa, lazima wasafiri tu- Ndugai

Comments

comments